Join our Telegram channel for instant songs and free Downloads Subscribe Now!

MAMBO 10 AMBAYO HUENDA HUKUYAJUA KUHUSU ALIKIBA

Muziki Huru

MAMBO 10 AMBAYO HUENDA HUKUYAJUA KUHUSU ALIKIBA ‘KING KIBA’

Alikiba ni miongoni mwa majina makubwa yaliyodumu kwa muda mrefu kwenye muziki wa Bongo Fleva, akiwa amejijengea heshima ndani na nje ya Tanzania.

Lakini pamoja na umaarufu wake, kuna baadhi ya mambo kuhusu safari yake ya muziki na maisha yake ambayo huenda hukuyajua.

1. Aliwahi kusajiliwa na Coastal Union 

Mbali na muziki, Alikiba aliwahi kuwa na uhusiano na soka, ambapo alisajiliwa na klabu ya Coastal Union kwa msimu wa 2018/19.

2. Aliwahi kukaa muda bila kutoa hit kubwa 

Kabla ya kurejea kwa kishindo na wimbo “Mwana” mwaka 2014, Alikiba aliwahi kukaa kipindi bila kutoa muziki uliokuwa na impact kubwa kama ilivyokuwa awali.

3. “Mwana” ilimrudisha kwa kishindo 

Baada ya kurejea kupitia “Mwana,” Alikiba alipata mafanikio makubwa na mwaka 2015 akafanikiwa kupata tuzo mbalimbali kwenye Tanzania Music Awards.

5. Aliwahi kuwa sehemu ya project ya One8 

Alikiba aliwahi kushiriki kwenye project ya One8, iliyowakutanisha wasanii mbalimbali kutoka Afrika pamoja na staa wa Marekani R. Kelly.

5. King Kiba ana uwezo wa kupiga piano

Mbali na kuimba na kuandika nyimbo, Alikiba pia amewahi kutajwa kuwa na uwezo wa kupiga piano, jambo linaloonyesha upande mwingine wa kipaji chake cha muziki.

6. Alishinda MTV EMA mwaka 2016

Mwaka 2016 ulikuwa muhimu kwenye safari yake ya kimataifa baada ya Alikiba kushinda tuzo ya MTV Europe Music Awards (MTV EMA) – Best African Act.

7. Alisaini mkataba na Sony Music Entertainment

Katika mwaka huo huo wa 2016, Alikiba alisaini mkataba na Sony Music Entertainment, hatua iliyoongeza zaidi nafasi yake kwenye soko la muziki wa kimataifa.

8. Alikaa takribani miaka 10 kabla ya kumshirikisha tena msanii wa kike

Baada ya kufanya wimbo “Single Boy” na Lady Jaydee mwaka 2012, ilipita takribani miaka 10 kabla ya Alikiba kumshirikisha tena msanii wa kike kwenye wimbo wake, kupitia “Yalaiti.”

9. Alikiba pia ni mwandishi wa nyimbo

King Kiba si mwimbaji pekee, bali pia anajulikana kwa uwezo wake wa kuandika nyimbo. Ameripotiwa pia kuhusika katika uandishi wa wimbo “Zali” wa Dully Sykes.

10. Aliingia zaidi kwenye biashara ya media

Mwaka 2024, Alikiba alipanua shughuli zake kwenye sekta ya media kwa kuzindua Crown FM 92.1, ikiwa ni hatua nyingine nje ya muziki.

SWALI KWA MASHABIKI

Kati ya haya 10, ni jambo gani kuhusu King Kiba ambalo ulikuwa hulijui kabisa? Tuambie kwenye comments, tupate kujua ni wangapi wamejua leo!

Post a Comment

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.